KIKOSI CHA FREE STATES BILA NGASSA...
Wakongwe Kaizer Chiefs wameifunga Free State Stars kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) katika mechi iliyopigwa jijini Johannesburg.

Chiefs wameishinda Free State anayoichezea Mtanzania Mrisho Ngassa ambaye hata hivyo dakika zote 90 alikuwa kwenye benchi.
 
KIKOSI CHA KAIZER CHIEFS KILICHOIMALIZA FREE STATE STARS YA NGASSA...
Ngassa aliendelea kubaki kwenye benchi huku Kocha Kinah Phiri akifanya mabadiliko yote matatu bila ya kumteua.
Bao safi la Siphiwe Thshabalala lakini mawili mawili ya kujiunga ndiyo yalichangia kuiua Free State.
 
PHIRI AKIMKABIDHI NGASSA JEZI BAADA YA KUTUA FREE STATES...
Kutokana na kipigo hicho, timu ya Ngassa sasa inashika mkia katika PSL baada ya kucheza mechi mbili na kupoteza zote
WALIOKUWA BENCHI:
Diakite, Makhaula, Angula, Somaeb, Thethani, Ngasa, Fileccia

AddThis

 
Top