Mwnamuziki
nyota na mkongwe mwenye asili ya Congo King Blaise Mfalme wa band ya Fm
Academia amewashangaza watu wa media hasa watangazaji baada ya kuachia wimbo wa
dansi wenye dakika tano tu alafu mzuri sana
Wimbo huo
uitwao DADA HUYO ukiwa ni utunzi wake kupitia band yake ya fm academia umekuwa
gumzo kutokana na uzuri wa wimbo na uchache wa dakika kitu ambacho
kimewashangaza watangazaji wengi wa vyombo mbali mbali vya habari kwani
walishazowea nyimboza dansi nilazima ziwe na dakika nyingi
Wengi
tunafahamu kuwa mara nyingi nyimbo za dansi zimekuwa na kawaida ya kuwa ndefu
kuanzia dakika nane hadi kumi na zaidi ,lakini kwa sasa mambo yameanza
kubadilika kwa nyimbo za dansi kufupishwa
Hilo
limejidhihirisha kupitia wimbo huu wa DADA HUYO utunzi wa king Blaise
Zipo band
ambazo zimejaribu kutoa nyimbo zenye dakika chache lakini hazikuweza kuwa gumzo
au kuonyesha dalili ya kupendwa na kushtua watangazaji kama wimbo huu wa dada
huyo ambao upo hewani kwa sasa
Baadhi ya
watangazaji waliyosikia wimbo huu na kucheza radioni walishtuka na kusema kuwa
kumbe inawezekana wimbo wa dansi kuwa mfupi na ukawa mzuri (kama kushtuka na kushangaa)
Lakini kwa
upande wake mtunzi wa wimbo huu King blaise amesema alitunga wimbo huu muda
mrefu na kama angerekodi kadiri ya alivyo utunga basi ungekuwa na dakika kumi
au kumi na mbili
“unajua
wimbo nimetunga zamani sana na kama ningerekodi kama nilivyo utunga ungekuwa na
zaidi ya dakika kumi au kumi na mbili ,lakini sasa mambo yanabadilika kwa hiyo
mimi kama mwanamuziki lazima nisome alama za nyakati kwa kujua soko la muziki
sasalipovipi na mashabiki wanataka nini kwa wakati gani”
Nao Baadhi
ya mashabiki wa dansi kupitia mitandao ya kijamii wamesema kuwa wameshawahi
kusikia nyimbo za dansi zenye dakika chache lakini hazina kiwango kama wimbo
huu wa DADA HUYO
Wimbo wa DADA HUYO umetungwa na King Blaise umerekodiwa katika ya alain mapigo lakini waliyotia rap ni Gseven na Bodack Nduala Mp3 huku gitaa la solo likicharazwa na mkongwe Christian mene Mukambilwa
Wimbo huu
kwa sasa upo katika mitandao ya kijamii ikiwemo you tube ila official video is
coming soon
TAZAMA
SIMPLE VIDEO HAPA CHINI