Mwanariadha maarufu wa Uingereza, Mo Farah mwenye asili ya Somalia ameshinda mbio za ubingwa wa IAAF zinazofanyika jijini Beijing, China huku akiwaacha wanariadha wa Kenya ambao walionekana watakuwa tatizo kwake.

Farah ameshinda mbio ndefu za mita 10000 akiwaacha Wakenya watatu ambao walikuwa wamemzunguka ikionekana walikuwa wakifanya juhudi mmoja wao aibuke na ushindi.
Hata hivyo, Farah alionekana kuwa fundi zaidi yao kwa kuwazidi ujanja na kuibuka mshindi katika hatua za mwisho.






AddThis

 
Top