![]() |
MGETA (KULIA) KATIKA TANGAZO LA MECHI HIYO KABLA HAIJACHEZWA. |
Timu
ya daraja la tano nchini Ujerumani anayochezea Mtanzania Emily Mgeta
imeanza ligi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Heiningen.
Mgeta
ameichezea timu yake hiyo ya Neckarsulmer dakika 70 ikiwa ni mara yake
ya kwanza kucheza Ligi ya Ujerumani inayotambulika kama Verbandsliga.
Kikosi hicho cha Neckarsulmer kilikuwa ugenini lakini kilifanikiwa kufunga bao kila kipindi.
"Tumeshinda kwa mabao mawili, umekuwa ni mwanzo mzuri ingawa katika dakika ya 70 nilitolewa," alisema.
"Tumecheza vizuri kabisa tena tukiwa ugenini, sasa tunarudi kujiandaa na mechi ijayo," alisema beki huyo wa zamani wa Simba.