Balozi Dr. Augustine Mahiga (kushoto) akiwa na mkewe, Elizabeth Mahiga (katikati) na kada wa CCM Eng. Lucas B.Chogo.
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.
ALIYEKUWA  Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dr. Augustine  Mahiga,   amesema anazo sifa zote za kumfanya kuwa rais bora wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyasema hayo hapo jana katika Idara ya Habari (Maelezo) alipokuwa akitangaza nia ya kugombea urais kupitia (CCM) akisisitiza ameamua kufanya hivyo ili kurudisha mmomonyoko wa maadili ambao umepotea na miongoni mwa watendaji wa serikali  na kusababisha  kuongezeka kwa  vitendo vya rushwa na ufisadi.
“Ubadhirifu na ufisadi katika taifa linaloendelea unahitaji kupigwa vita na kiongozi imara ili kujenga nchi yenye demokrasia ya kweli pamoja na kuleta  maendeleo ya wananchi.
“Chama changu cha CCM kikiniteua nitawatumikia wanachi katika kujenga uchumi imara miongoni mwao na nitaondoa matabaka yanayotokana na ubadhirifu wa mali za umma,” alisema.
NA DENIS MTIMA/GPL

AddThis

 
Top