Dustan Shekidele, Moro
K
ichapo! Katika hali ya kushangaza, kigogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani hapa, Fatuma Mussa amejikuta akipokea mkong’oto wa aina yake kisha kunusurika kuchomewa nyumba moto na raia wenye hasira kali akidaiwa kumfanyia ukatili ‘hausigeli’ wake aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Emmanuel.
 IMG_8888
 akiminyiwa kichapo
IMG_8866
Kigogo huyo akijifunika kukwepa kupigwa picha.
Tukio hilo la kusikitisha lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri Mtaa wa Mfuru Kata ya Tungi mjini hapa, wikiendi iliyopita, majira ya asubuhi baada ya raia hao kuchoshwa na ukatili huo.
Wakati kigogo huyo anayekusanya ushuru akimtwanga hausigeli huyo huku akimtukana, alikuwa akishirikiana na mama yake aliyefahamika kwa jina la Mama Fatuma.
IMG_8837
Hausigeli akilia kwa manyanyaso ya kigogo huyo.
Kufuatia sakata hilo, watu walifanya jitihada za kumtoa hausigeli huyo na walipofanikiwa ndipo wakamshambulia kigogo huyo na mama yake kwa kuwashushia kipigo ‘hevi’ huku wakitaka kuchoma moto nyumba yake kisha waliwapeleka kwenye ofisi ya serikali ya mtaa, kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kutuliza ghasia.
IMG_8894Polisi walipofika waliwabeba msobemsobe watuhumiwa hao na hausigeli huyo aliyekuwa akiangua kilio kwa maumivu aliyopata kisha kuwapeleka Kituo Kiuu cha Polisi ambapo walipelekwa kwenye Dawati la Jinsia chini ya Afande Sophia.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, hausigeli huyo alikuwa na haya ya kusema: “Kama ni mateso basi haya yamezidi kipimo, nawashukuru wananchi kwa kuninusuru.”
Hata hivyo, polisi waliwaachia watuhumiwa hao kwa sharti la kumlipa hausigeli huyo stahiki yake na kumrudisha kwa wazazi wake.

AddThis

 
Top