ray-c-6
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.

MSANII mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ atayaweka hadharani maisha yake ya utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kumpata mfadhili kutoka Ujerumani ambaye atarekodi historia yake katika mkanda wa video.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Ray C alisema anashukuru Mungu kwa kumleta mfadhili huyo ambaye atarekodi maisha aliyopitia, jinsi alivyokuwa akifanya mpaka kupata hela ya kununua unga kitu alichodai kitawasaidia sana vijana wengi.
“Nimekuwa nikilia kwa muda mrefu kupata msaada, sasa naona Mungu amesikia kilio changu, pamoja na kurekodi ‘documentary’ yangu, pia natarajia kufungua taasisi yangu ya Ray C Foundation,” alisema.

AddThis

 
Top