Sean
O'Driscoll yuko tayari kuachia nafasi yake ya ukocha wa timu ya Taifa
ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 19 na kujiunga na benchi la
ufundi la Liverpool.
Bosi wa Majogoo, Brendan Rodgers amempendekeza Sean kuwa msaidizi wake namba moja.
Kwa
muda mrefu sasa, Liverpool wamekuwa wakitafuta kocha wa kumrithi Colin
Pascoe na Mike Marsh ambao wamefukuzwa kazi kutokana na matokeo mabaya
ya klabu hiyo msimu uliopita.
Kocha wa kikosi cha vijana chini ya miaka 16 cha Liverpool , Pepijn Lijnders amepandishwa timu ya kwanza, huku O’Driscoll akitarajia kuungana naye.
Kwa mujibu wa Rodgers, O’Driscoll ndiye kocha bora nchini England na amewahi kuzifundisha vizuri timu za Doncaster Rovers, Crawley Town, Nottingham Forest na Bristol City.
O'Driscoll alijiunga na FA mwezi septemba kwa ajili ya kufundisha timu za vijana.
Wakati huo huo, Mike Marsh ameripotiwa kuwa na mpango wa kujiunga na Sheffield kesho Jumatano.