Timu
ya Taifa ya Chile imetinga nusu fainali ya michuano ya mataifa ya
America kusini (Copa America) baada ya kuitandika Uruguay goli 1-0
katika mechi ya robo fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye
uwanja wa Santiago.
Goli pekee la wenyeji Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika dakika ya 81'.
Dakika
ya 63' Uruguay ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Edinson Cavani
kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kuoneshwa kadi ya kwanza ya njano kwa
kosa la kumtukana mwamuzi wa mechi.
Wakati
huo huo beki Jorge Fucile naye alioneshwa kadi ya pili ya njano na
hatimaye nyekundu katika dakika ya 90' baada ya kumchezea vibaya Alexis
Sanchez wa Chile.
Kwa matokeo hayo, Chile itacheza nusu fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya robo fainali itakayowakutanisha Bolivia na Peru.