Mayasa Mariwata

MSANII wa filamu Bongo, Lucy Komba ambaye amehamishia makazi yake nchini Denmark kwa mumewe, imebainika kuwa kilichomfanya aolewe na mzungu huyo ni kutokana na kufuata masilahi na siyo mapenzi ya dhati kwa kuwa bado hayupo tayari kuzaa naye.
Msanii wa filamu Bongo, Lucy Komba akiwa na mumewe siku ya harisi yao.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na msanii huyo zilieleza kuwa, Lucy mpaka sasa hafikirii hata kidogo suala la kuzaa na mzungu huyo, kwa kuwa kilichompeleka huko si upendo wa dhati hivyo suala la kuzaa naye halipo kabisa kichwani mwake.
Baada ya kupata ubuyu huo, paparazi wetu alimsaka Lucy kwa njia ya simu ambapo alisema anatarajia kuanza kusoma akishamaliza atamzalia mumewe watoto watatu.

AddThis

 
Top