Manchester United wameweka mezani ofa ya kwanza ya paundi milioni 35 wakiitaka saini ya beki wa Real Madrid aliyeomba kuondoka Bernabeu, Sergio Ramos.
Ramos alikutana na maafisa wa Real Madrid jana asubuhi na kuomba kuondoka.
Mkurugenzi mkuu wa Real Madrid, Jose Angel Sanchez alikaa na mchezaji pamoja na kaka yake ambaye ni wakala wake pia, Rene Ramos katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo,  Valdebebas, lakini badala ya kuzungumzia mkataba mpya, mlinzi huyo aliiomba klabu hiyo kufungua mazungumzo na Manchester United.
Hata hivyo imefahamika kwamba dili hili halihusiani na la Golikipa, David de Gea anayetaka kutua Real Madrid kutokea Man United majira haya ya kiangazi.

AddThis

 
Top