Waziri mkuu wa Australia, Tony
Abbott, ameyaomba mataifa ya Asia-Pacific kuungana ili kusaidia katika
vita dhidi ya makundi ya kigaidi.
Abbot amewaambia mawaziri kutoka kwa mataifa 25 katika mkutano wa kikanda unaofanyika mjini Sydney kuhusu usalama.Amesema kuwa kundi la Islamic State lina nia ya kutawala dunia, huku akielezea kuwa hilo ni kundi la mauti, lenye mafunzo mabaya ya itikadi kali.
Waziri huyo mkuu ameongeza kuwa Australia imeamua kuzuia raia wa nchi hiyo kujiunga na wanamgambo wa Islamic State
White House sasa inasema kuwa ina imani mikakati yake ya kutoa mafunzo kwa vikosi vya kiusalama vya Iraq na kuwaingiza jeshini wapiganaji wa kikabila wa Sunni, itafaulu katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.