Mbunge
wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu akiwa na mwanaye.
BAADA ya Mbunge wa Mbeya Mjini
kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mheshimiwa
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuripotiwa kumfikisha mahakamani mzazi mwenziye,
Faiza Ally, Juni 19, mwaka huu akitaka mahakama impe haki ya kumlea
mtoto wao, Sasha (2), sakata limeisha kwa Sugu kukabidhiwa mtoto amlee.
Katika hukumu ya kesi hiyo iliyosomwa
juzi Jumanne huku upande wa mlalamikaji ambaye ni Mhe. Sugu
ukiwakilishwa na mwanasheria wake kutokana na Sugu kuwa bungeni mjini
Dodoma, mdaiwa Faiza alionekana kubanwa na baadhi ya vielelezo huku
suala la maadili likiwa ndiyo sababu kuu ya kumkosesha haki ya kumlea
mtoto huyo.
HUKUMU ILIVYOTOLEWA
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi
Patrick Vaginga wa Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sina jijini Dar, alisema
baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili, yaani mlalamikaji ambaye
ni Sugu na mlalamikiwa ambaye ni Faiza, mahakama hiyo imempa Sugu haki
ya malezi ya mtoto kutokana na upungufu wa malezi ya mama ambaye ni
Faiza.
FAIZA AKIRI
Hakimu Vaginga alisema kuwa kutokana na
mlalamikiwa kukiri vielelezo vyote vya picha za nusu utupu ambavyo
mlalamikaji, Sugu aliviwasilisha dhidi yake, mahakama imeona kumwacha
mtoto kwa mama kutaathiri makuzi kwa kuwa mtoto hujifunza haraka akiwa
katika umri huo hasa kupitia mama.
VILIVYOMPONZA FAIZA
Hakimu huyo alivitaja baadhi ya vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na Sugu kuwa ni picha ya Faiza akiwa amevaa pampasi.
Picha hiyo ilipigwa kwenye ‘bethidei’
yake, Desemba 18, mwaka jana. Picha akiwa amevaa shati tu ambayo
alipigwa kwenye shoo ya Zari iliyojulikana kwa jina la Zari All White
Party iliyofanyika Mei Mosi, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar.
Hakimu Vaginga aliitaja picha nyingine
kuwa ni ile ya kigauni kifupi kilichoacha makalio nje. Alipigwa kwenye
hafla ya Tuzo za Kili Music iliyofanyika Juni 13, mwaka huu katika
Ukumbi wa Mlimani City.
FAIZA AANGUA KILIO MBELE YA HAKIMU
Mara baada ya hukumu hiyo kusomwa, Faiza
alishindwa kujizuia na kuangusha kilio mfululizo mbele ya hakimu,
ikabidi atoke nje akisindikizwa na askari ili kuwezesha mahakama
kuendelea na kesi nyingine.
FAIZA BAADA YA KUNYAMAZA KULIA
Baadaye akiwa ameacha kulia, waandishi
wetu walimfuata Faiza akiwa ndani ya gari na kumuuliza alivyojisikia
kufuatia hukumu hiyo, akasema:
“Siwezi kusema lolote lakini Mungu
anajua. Mimi siwezi kuishi bila mwanangu Sasha. Nawaambia nitakufa.
Sidhani kama wiki itapita mimi sijafa.”
Waandishi: Deogratius Mongela, Chande Abdallah na Imelda Mtema.