Chande Abdallah
Bahati ilioje! Kibaka mmoja aliyejulikana kama Baba Hawa, mkazi wa Sinza Kamanyola jijini Dar juzikati nusura auawe kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira baada ya kunaswa akiiba kinyonyeo cha kompyuta (flash) kwenye duka moja la vifaa vya ofisini (stationery) lililopo Bamaga, Mwenge.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa duka hilo, mtu huyo aliingia kwa mbwembwe kama mteja wa kawaida akiomba kutolewa fotokopi ya makaratasi yake ambayo yalionesha mahesabu ya chuo kikuu.
Wakiongea kwa kupokezana, wafanyakazi hao walidai wakati wakimhudumia, alionekana kuwa macho juujuu huku akishtuka kila alipotazamwa,  jambo lililowafanya wamtilie mashaka hivyo kukagua vifaa vyao............

AddThis

 
Top