Mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid itashuka Uwanjani hapo kesho nchini Uingereza kuwakabili vijana wa kocha Mauricio Pochettino, Tottenham Hotspur katika mchezo wa kundi H.

Madrid inarejea Uingereza kucheza hatua hiyo ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya huku ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kutopoteza michezo mitano iliyopita katika ardhi nchi hiyo.
Real imeshindamichezo mitatu na kutoka sare miwili ikiwa Uingereza msimu wa mwaka 2010/11 ikichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham katika hatua ya robo fainali bao pekee la Cristiano Ronaldo.
Msimu wa mwaka 2012/13 dhidi ya Manchester City hatua ya makundi mchezaji Karim Mostafa Benzema akiisawazishia Whites na kuchomoza na sare ya 1-1.
Katika hatua ya 16 bora dhidi ya United ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 wakati Modric na Ronaldo wakiiwezesha timu hiyo kuchomoza na ushindi huo.
Mwaka 2014, the Whites ikachomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield hatua ya makundi wakati waliyofunga ni Straika Karim Benzema na Cristiano Ronaldo.
Na mara ya mwisho kuwasili Uingereza ikicheza dhidi ya Manchester City na kutoka sare tasa ya bila kufungana mwaka huo huo.
Tottenham Spurs na Real Madrid wanakutana katika mchezo wa marudiano baada ya ule wa wali uliyopigwa Santiago Bernabeu timu hizo kutoka sare ya 1-1 mabao yakifungwa na Harry Kane upande wa Spurs na Cristiano Ronaldo kwa Madrid matokeo ambayo yaliifanya timu hiyo kutoka Uingereza kuongoza kundi H kwa kufunga magoli mengi ya ugenini kuliko wapinzani wao.

AddThis

 
Top