Kocha wa zamani wa Ndanda FC na Mbeya City, Meja Mstaafu, Abdul Mingange ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam FC.
Mingange anachukua nafasi ya Idd Nassor Cheche, ambaye tangu Januari mwaka huu amepandishwa kuwa kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa, chini ya Mromania, Aristica Cioaba.  
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kwamba Mingange ni kocha mzofu na mwenye rekodi nzuri ya kufanya kazi na wachezaji vijana.
Idd Nassor Cheche (kulia) sasa ni Kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa ya Azam FC chini ya Mromania, Aristica Cioaba 
“Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC kwa pamoja na uongozi, imezingatia sifa za Meja Mingange kulingana na mahitaji ya klabu kwa mwalimu wa U-20. Niseme tu kwamba, tuna matarajio makubwa kwa Meja Mingange,”amesema Maganga.
Pamoja na hayo, Maganga amesema uongozi umeridhishwa na maendeleo ya Iddi Cheche kama kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa.
“Pia uongozi umefurahishwa na utendaji mzuri wa Cheche kama kocha Msaidizi na unamtakia kila la heri,”amesema.

AddThis

 
Top