Katika kile ambacho kinaonekana kuwa hali ya mambo kwa beki wa kulia wan Simba, Shomari Kapombe siyo nzuri,
kuna tamko limetolewa kuwa kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo akatemwa katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Novemba 15, mwaka huu.
Kapombe alisajiliwa na Simba akitokea Azam FC lakini tangu atue klabuni hapo ameshindwa kupata nafasi ya kucheza muda mrefu kutokana na kuandamwa na majeraha kwa miezi kadhaa.
Katika kile kinachoonekana wazi mchezaji huyo ataondolewa klabuni hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe amenukuliwa akisema Kapombe anatakiwa kucheza na kama anaona afya yake haipo sawa ni vema akakaa pembeni  ili akipona arejeshwe kikosini.
Akifafanua zaidi, Hans Poppe alisema: “Vipimo havidanganyi, yeye kama anaona hawezi kucheza basi akae pembeni, siyo anakaa anakula mshahara wa bure.
“Kama amepona acheze, kama hataki basi aondoke, majeruhi gani ambaye haponi muda wote huo!”
Alipoulizwa kuhusu vipimo vinavyosema, alisema: “Vipimo vinaonyesha ameshapona vizuri, yeye ana uwoga wake tu, labda anaogopa ataumia, msimamo wetu ni yeye mwenyewe aamue acheze au aondoke.”

AddThis

 
Top