Kipa mkongwe amethibitisha baada ya mechi ambayo walipata sare dhidi ya Sweden kuwa ndiyo mechi yake kwa timu ya taifa Italia.
Kipa huyo, Gianluiggi Buffon amethibitisha kuwa amestaafu kuichezea timu ya Italia baada ya kushindwa kufuzu Kombe la Dunia 2018.
Kipa huyo gwiji aliwahi kuashiria kuwa anakaribia kustaafu kuichezea Azzurri baada ya michuano ya Urusi. Lakini Italia wametolewa kwenye michuano hiyo baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Sweden mjini Milan Jumatatu, kwani wageni wao walisonga mbele kwa jumla ya 1-0 ushindi waliopata mechi ya kwanza.
Ni mara ya kwanza kwa mabingwa wa mara nne wa dunia kukosa michuano hiyo tangu 1958.
Nyota huyo wa Juventus hajahuzunishwa na kumalizika kwake kwa soka Italia bali matokeo yaliyoathiri soka la Italia.
"Inasikitisha," Buffon aliliambia Rai Sport akibubujikwa na machozi.
"Si kwangu, bali kwa maendeleo ya soka, kwa sababu tumeshindwa kupata kilicho muhimu kwa ajili ya nchi yetu. Hayo ndiyo majuto pekee niliyo nayo na kwa yakini si kwa sababu nastaafu, kwa sababu hili litapita na ni sawa.
Gianluigi Buffon Italy
"Ni aibu kwenye mechi yangu ya mwisho kwani nimemaliza kwa kushindwa kufuzu Kombe la Dunia. [Lakini] upo mustakabali bora kwa soka la Italia, kwani tunayo mengi ya kujivunia, uwezo, nia, na baada ya matokeo mabaya tutatafuta njia ya kutokea.
"Naondoka kwenye kikosi cha Italia ambacho kitaweza kujitetea chenyewe."
Buffon anastaafu soka timu ya Italia akiwa amecheza mechi 175 katika kipindi cha miongo miwili, na kushinda Kombe la Dunia 2006 Ujerumani. Mkongwe huyo wa miaka 39 ameiwakilisha Italia kwenye michuano mitano Kombe la Dunia, na minne Ulaya na Kombe la Shirikisho mara mbili.

AddThis

 
Top