Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Patrice Evra ameondoka klabu ya Marseille na amepigwa marufuku kushiriki mashindano ya Uefa msimu huu baada ya kumpiga teke shabiki wa klabu hiyo ya Marseille kabla ya mechi kuanza.
Mchezaji huyo aliyewahi kuchezea Monaco na Juventus amepigwa marufuku na shirikisho hilo la soka Ulaya hadi Juni 2018, mwezi ambao mkataba wake Merseille ungemalizika.
Amepigwa faini ya euro 10,000 (£8,829).
Evra, 36, alimpiga teke shabiki aliyekuwa karibu na uwanja wachezaji walipokuwa wanapasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mechi ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya Vitoria Guimaraes tarehe 2 Novemba.
Beki huyo wa Ufaransa alijiunga na Marseille Januari 2017 kutoka Juventus, klabu ambayo alikuwa ameichezea kwa misimu mitatu baada ya kuondoka Old Trafford.
Evra ameondoka Marseille kwa maafikiano na klabu hiyo.
Evra alimpiga kichwani shabiki wachezaji wakipasha misuli moto uwanjani kabla ya kuanza kwa mechi ya ugenini dhidi ya Vitoria Guimaraes katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Marseille walilazwa 1-0 mechi hiyo.
Picha za video zinamuonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenye miaka 36 akiruka juu na kumpiga teke shabiki huyo.
Evra, ambaye alikuwa ametajwa kwenye benchi, alifukuzwa uwanjani hata kabla ya mechi kuanza.
Marseille walianza wakiwa na wachezaji 11.
Gazeti la Ufaransa la L'Equipe limesema mashabiki wa Marseille walikuwa wamemzomea Evra kwa karibu nusu saa wachezaji walipokuwa wakijiandaa kwa mechi.
Evra alikuwa ameenda kuzungumza nao kuwatuliza lakini badala ya kupunguza kelele, wakazidisha na hali ikabadilika ghafla.
Mwanahabari wa Ufaransa Julien Laurens amesema Evra - ambaye mara nyingi hupakia video za ucheshi kwenye mitandao ya kijamii - alitukanwa na kuambiwa: "Endelea kuandaa na kusambaza video zako, lakini uache kucheza kandanda."

AddThis

 
Top