Mchezaji
wa Tottehham, Harry Kane anaongoza orodha ya washambuliajo, wakati John
Stones wa Everton ndiye roho ya ulinzi kwenye kikosi hicho, huku
Francis Coquelin na Hector Bellerin wa Arsenal nao wakijumuishwa.
Kitu
cha kuvutia ni kwamba; hakuna mchezaji yeyote kutoka ligi kuu ya
Hispania, La Liga, wakati ligi ya Italia, Seria A imeingiza wachezaji
wengi.
Bundesliga ya Ujerumani imeingiza wanandinga wawili, wakati wachezaji wa mwisho wametoka ligi ya Ufaransa, Ligue 1.
Wachezaji
wengi walioingia kwenye kikosi hiki wanatarajia kucheza michuano ya
Ulaya ya vijana chini ya umri wa miaka 21 inayoanza kutimua vumbi wiki
ijayo mjini Prague.
Timu ya taifa ya vijana ya Ujerumani ndio inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, ikifuatiwa na England na Ureno.
Kikosi bora cha vijana cha ulaya msimu wa 2014/2015 kilichotajwa na The Marca hiki hapa chini
Timo
Horn; Hector Bellerin, Daniele Rugani, John Stones, Baba Rahman; Mirko
Valdifiori, Francis Coquelin; Felipe Anderson, Paulo Dybala, Nabil
Fekir; Harry Kane
Kabla hujauliza, hatuna majibu kivini na kwanini mchezaji mwenye miaka 29, Mirko Valdifiori ameingia kwenye orodha ya Marca!?