FILAMU inayoelezea maisha ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronadlo kwa mwaka uliopita inatarajia kutoka baadaye mwaka huu.
Watengenezaji
wa filamu hiyo wamesema Ronaldo ndiye mhusika mkuu na wanaamini
itawavutia watu wengi kwani imeeleza vitu vingi kuhusu maisha ya
mchezaji huyo bora wa dunia.
Filamu
hiyo inatarajia kuonesha wapi alipanda na kushuka katika maisha yake ya
soka mwaka uliopita na mpaka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia,
FIFA Ballon d'Or kwa mara ya tatu mwezi Januari mwaka huu.
Pia Filamu hiyo inatarajia kuonesha upinzani mkubwa kati ya Mreno huyo mwenye miaka 30 na nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Wakati
Ronaldo anatoka kapa msimu huu wa La Liga, Lionel Messi ameiwezesha
Barcelona kuchukua makombe matatu kwa maana ya La Liga, Copa del Rey na
Uefa Champions League.
Jina
la Filamu hiyo litatoa jibu kwa mashabiki wengi wa soka duniani ambao
wamegawanyika juu ya nani ni mchezaji bora wa dunia kati ya Ronaldo na
Messi.


Tayari Ronaldo amethibitisha kuwepo kwa filamu hiyo;
I’m happy to confirm that there’s a film being produced about me. Stay tuned for more info at @RonaldoFilm