BINGWA
wa dunia wa ngumi za uzito wa juu 'heavyweight', Deontay Wilder
anaamini anaweza kurithi mikoba ya Floyd Mayweather Jr ya kuwa
mwanamasumbwi anayetisha zaidi duniani.
Mmarekani
huyo amefanikiwa kutetea ubingwa wa WBC katika ardhi ya Alabama,
Marekani baada ya kumtandika bondia Eric Molina mwishoni mwa juma
lililopita.
Licha ya kuwepo kwa mabondia bora wa dunia wakiwemo mabingwa wa ngumi za uzito wa juu wa IBF, WBA na WBO kama vile Wladimir Klitschko, Anthony Joshua , Wilder anaamini yeye ndiye bondia bora zaidi duniani.
Bondia huyo mwenye miaka 29 amesema: "Floyd
Mayweather anaelekea kumaliza maisha yake ya ngumi. Inabidi nichukue
nafasi yake. Naamini naweza kuwa bondia mpya mwenye mvuto zaidi duniani"