Jurgen Klopp anatamani kufundisha ligi kuu England akimaliza mapumziko yake, hii ni kwa mujibu wa wakala wake.
Kocha
huyo Mjerumani aliondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu baada
ya kukaa miaka saba Bundesliga akiwaongozo kutwaa makombe mawili ya
Ligi kuu, Kombe la Ujerumani na alifika fainali ya Uefa Champions
league.
Wakala
wake, Marc Kosicke amesema mipango ya Klopp kwasasa ni kupumzika
kufundisha mpira ili kuchaji kichwa chake, lakini atakaporudi kwenye
kazi hiyo anatamani kufundisha timu ya England.
Akingumza
na SPOX, Kosicke amesema: "Ligi kuu ya England inavutia sana na
hatufikirii tu timu nne za juu kwasababu kuna baadhi ya timu kubwa za
chini".
Bila
shaka hizi ni taarifa njema kwa klabu za Liverpoool na Manchester City
ambazo zimeonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Klopp.