Goli
tatu ‘hat-trick’ ya Paolo Guerrero ‘Predetor’ dhidi ya Bolivia
inaipeleka Peru kiulaini kwenye nusu fainali ya michuano ya Copa America
2015 inayozidi kushika kasi huko nchini Chille baada ya Peru kuibuka na
ushindi murua wa goli 3-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa usiku
‘mwingi’ wa Alhamisi kuamkia leo (Ijumaa).
Zilimchukua
dakika 20 tu Guerrero ambae ni straika wa klabu ya Corinthians
kupachika bao la kwanza na kuanza kuitafuta hat-trick yake kwenye
michuano hiyo akiunganisha krosi safi kutoka kwa Romel Quinonez. Dakika
tatu baadae mkali huyo alizama tena wavuni kupiga goli la pili kabla
hajashindilia msumari wa mwiso dakika 16 kabla ya mchezo kumalizika.
Mshambuliaji wa zamani wa Wigan Athletic Marcelo Moreno aliipatia
Bolivia goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati na mchezo huo
kumalizika kwa Peru kutinga fainali kwa ushindi wa goli 3-1.
Ushindi
huo unaifanya Peru ikumbane na wenyeji Chile kwenye mchezo wa nusu
fainali ya mashindano hayo ya Copa America kwenye dimba la Santiago siku
ya Jumatatu Juni 29 mwaka huu kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza hatua
ya fainali.