Mchezaji
Jonas Mkude wa Simba SC ameondoka jana mchana kwa ndege ya South Africa
Airways kwenda nchini Afrika Kusini kwa majaribio katika klabu ya
Bidvest Wits.
Akifanya
mahojiano na Tovuti rasmi ya Simba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) Mkude amewaomba Watanzania wazidi kumwombea ili
aweze kufuzu majaribio.
Mkude
ameondoka akiwa na Baraka zote za Klabu ya Simba, Rais wa Simba Evans
Aveva alisema “Simba inamtakia kila la kheri Mkude kwenye majaribio yake
kwenye Klabu ya Bidvest Wits huko Afrika Kusini na hili liwe fundisho
kwa vijana wengine kuendeleza vipaji ili waweze kucheza mpira kwenye
ligi za Nchi nyingine kubwa hivyo kukuza upeo na vipaji Zaidi katika
soka”
Mkude
alizaliwa Desemba 3, 1992 Kinondoni B na kuanza soka lake akiwa mlinda
mlango hadi kuwa kiungo wa kutegemewa. Aidha alianza elimu ya msingi
mwaka 1998 katika shule ya Hananasif na kumaliza mwaka 2005