Kiungo
wa Juventus, Paul Pogba yupo kwenye rada za klabu kubwa barani ulaya
ikiwemo Chelsea ambayo imeingia rasmi katika mbio hizo jana.
Kwa
mujibu wa Mwandishi maarufu wa Italia, Gianluca Di Marzio, Chelsea
wameshaanza kuwasiliana na Pogba kuangalia uwezekano wa kumsajili.
Real
Madrid, Barcelona, PSG na Manchester City zinahusishwa kuiwinda saini
ya nyota huyo kijana wa Vibibi vya Turin na kama atasajiliwa kuna
uwezekano wa kuwa mchezaji ghali zaidi wa wakati wote duniani.
Kutokana na kukosa nafasi ya kucheza Old Trafford, Paul Pogba aliondoka Manchester United na kutua Seria A mwaka 2012.
Jose
Mourinho tayari ana kiungo mahiri wa kati, Nemanja Matic na kama wazo
la kumsajili Paul Pogba litakamilika, watatengeneza muunganiko wa hatari
zaidi.