Wakala
wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo
amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa
itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP
Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo
hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.
“Katumbi
ameonesha bado anahitaji kumtumia katika kikosi chake kwenye michuano
ya champions league kwa maana hiyo makusudio yetu na matarajio yetu,
kunatimu moja kubwa ilitaka kumsaini kwa ‘Euro’ milioni moja lakini
bahati mbaya Katumbi alitaka amuache baada ya champions league kuisha”,
amesema wakala huyo wa Samatta.
“Kwahiyo
hili tulilitazama kwa upande wetu na kuona si jambo la busara kama ni
biashara hiyo ni bora abaki tu mpaka Januari ili aweze kuondoka kama
mchezaji huru na yeye kuweza kufaidika zaidi kama mchezaji na si
kuinufaisha TP Mazembe”, amesema.
“Kwa
kawaida, huwa sio vizuri sana kuviweka hivi vitu wazi, kwasababu ni
mapema, lakini kwa hiyo timu waliokuwa wanataka kutoa kiasi hicho cha
pesa ilikuwa siyo klabu ya Ulaya, ilikuwa ni klabu moja kubwa ya Afrika.
Na hicho ndio kitu kimojawapo kilichochangia kukataa ofa hiyo,
kwasababu kusudio letu kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Samatta
anacheza mpira Europe”, amefafanua.
“Sisi
tunataka hata kama pesa itakuwa ndogo lakini aende akacheze soka Ulaya
na kufungua milango kwa wenzake hata kama pesa ni ndogo. Tunauhakika
kama ataweza kucheza Ulaya kwa mwaka mmoja, basi anauwezo wa kutengeneza
pesa nyingi na timu kubwa zitakuwa zimeshaingia kwenye vita kubwa ya
kumsaka”, ameeleza.
“Tumeshapokea
ofa nyingi zaidi ya sita timu hasa zinamuhitaji, anahitajika na timu
nyingi. Tumepokea ofa kutoka Uswis, Ufaransa, Hispania na maeneo
mengine. Ni mchezaji ambaye yupo kwenye soko la Ulaya na timu
zinamuhitaji”, alimaliza.