Wakati
wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’
wanakutana leo kwenye hotel ya Tansoma kuzungumza na kocha wao mpya,
kiungo wa Simba SC na timu ya Taifa Jonas Mkude leo yeye anakwea ‘pipa’
na kutimkia Afrika Kusini kwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya Wits
University inayoshiriki liki kuu ya nchini humo
Afisa
habari wa klabu ya Simba Hajji Manara amesema, Simba wamempa baraka
zote kiungo huyo licha ya kuwa ameitwa kwenye timu ya Taifa, Manara
amesema tayari wamezungumza na kocha wa Stars Boniface Mkwasa kumpa
taarifa hiyo ya kiungo wao anaekwenda kufanya majaribio ya siku 14 (wiki
mbili).
“Tumempa
baraka zote za kwenda kufanya ‘trial’ lakini kumalizana naye ni mpaka
hapo badae atakapofuzu lakini tumempa baraka zote ‘full’, amepata
‘support’ ya Simba”, amesema Manara.
“Ni
kweli Mkude ameitwa kwenye timu ya Taifa lakini Mungu jaalia
tumeshazungumza na coach Charles Boniface Mkwasa na kumpa taarifa hiyo
kwamba Jonas anaondoka na yeye alikuwa hana taarifa hiyo lakini nadhani
haitakuwa tatizo kwake kwasababu anachoenda kukifanya pia ni nsehemu ya
‘program’ za TFF, lazima tuongeze ‘professionals’ wengi zaidi nadhani ni
baraka kwa nchi, wal Boniface hatakuwa na shida, ni mwalimu mweledi
sana”, ameeleza.
“Anakwenda
Wits University jina lao la utani wanaitwa ‘The clever boys’ ilishika
nafasi ya tatu nadhani kwenye msimu uliopita, atafanya majaribio ya siku
14 pale”, alimaliza Manara.