Wiki iliyopita tulizungumzia njia ya kuzuia mimba kwa kutumia Caps ambayo ni ndogo kuliko Diaphragms, tunaendelea kuchambua Progestogen kama ifuatavyo:
Chembechembe maalum ziitwazo Progestogen ni mchanganyiko wa Oestrogen na Progestogen, huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa mpangilio na kiwango maalum ili kuzuia mimba kutungwa.
Hufanya kazi kwa namna hii:
* Kwa kuzuia ovari kuangua mayai.
* Kwa kuzuia mbegu za mwanaume kulifikia yai (kwa kufanya majimaji ya ukeni kuwa mazito na kunata hivyo kuzuia mbegu ya mwanaume kupenya).
* Kwa kulizuia yai kujipachika kwenye kiota cha nyumba ya uzazi.
Chembe za kimaumbile
Tembe mchanganyiko - huwa ni kidonge cha dawa kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa chembe chembe za Oestrogen na Progestogen. Hii huzuia mimba kwa njia zote tatu tulizozitaja hapo juu na ikitumiwa itakikanavyo, vinategemewa kuzuia mimba kwa asilimia 99

AddThis

 
Top