Pamoja na kikosi cha Ruvu Shooting kushuka daraja, uongozi wa Maafande hao umefunguka kuwa haupo tayari kumpeleka beki wake, George Michael ‘Beki Katili’ katika timu yoyote hata kama ya jeshi kwa sababu bado wana mkataba naye.

Awali iliripotiwa kuwa JKT Ruvu ilipeleka maombi kwa ajili ya kumuomba beki huyo kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu ujao.
Ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire alifunguka kuwa beki huyo watashuka naye na hakuna timu ambayo inaruhusiwa kumchukua.
Bwire alisema kuwa katika kikosi chao kilichoshuka ni wachezaji sita tu ambao siyo waajiriwa wa jeshi ndiyo wapo huru baada ya mikataba yao kumalizika.

“Beki George Michael hatuna mpango wa kumtoa kwenda kwenye kikosi chochote ni mchezaji wetu halali na ana mkataba. Haijalishi kuwa ni timu ya aina gani huyu tutakuwa naye daraja la kwanza msimu ujao.


“Wachezaji ambao wapo huru mpaka sasa kwenye kikosi chetu wapo kama Juma Nade, Stephano Mwasyika, Juma Kijiko, Jerome Lambele na Salvatory Ntebe licha ya uongozi kutosema lolote kama wataendelea nao au la, kwa hiyo kama timu inahitaji ifanye mazungumzo na hao,” alisema Masau.

AddThis

 
Top