Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm
ametamka kuwa wachezaji wawili wa Ghana wakati wowote wanatarajiwa kutua nchini
kujiunga na kikosi hicho kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa
Afrika, mwakani.
Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache
tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati yao ya utendaji kuruhusu
klabu za ligi kuu kusajili wachezaji saba wa kimataifa.
Waghana hao, walitakiwa kuwepo kwenye
msafara wa kocha huyo akitokea Ghana kwenye mapumziko, lakini sheria za
wachezaji watano zikawazuia nyota hao kutua nchini kujiunga na Yanga.
Pluijm
hana taarifa ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kuongezwa kwenye timu shiriki
za ligi kuu, hivyo mara atakapopewa taarifa za kiofisi na viongozi haraka nyota
hao watatua.
Pluijm alisema, hawezi kutaja nafasi za
wachezaji hao watakaotua kuichezea Yanga, hivyo
mashabiki wasubirie kuwaona wakiwa uwanjani.
“Mimi
sina taarifa ya idadi ya wachezaji kuongezwa kufikia saba, mimi nasubiria
taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wangu na kama ni hivyo basi tutaongeza
wengine wawili wenye uwezo mkubwa tutakaowatumia kwenye michuano ya kimataifa.
“Wapo wachezaji wawili raia wa Ghana
niliotakiwa kuongozana nao hapa nchini tayari kwa kujiunga na Yanga, lakini
ikashindikana kutokana na TFF kugoma kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa.