Klabu
ya soka ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba imeendelea kulipiga danadana
suala la kumtangaza kocha mpya atakaechukua nafai ya Goran Kopunovic
ambapo uongozi wa timu hiyo umesema unatarajia kumtangaza mapema
mwanzoni mwa juma lijalo.
Afisa
habari wa klabu hiyo Hajji Manara amewataka wanachama na mashabiki wa
Simba kuendelea kuwa wavumilivu huhu akisema, tayari wameshampat kocha
kilichobaki ni kumtangaza tu.
“Kocha
tutamtangaza wiki ijayo, kwasababu tumeshampata, sisi wiki ijayo
tutamtangaza rasmi. Jumamosi mimi natoa ‘press release’ nikishatoa
tutawaeleza tutamtangaza lini, lakini Jumamosi natoa press release”,
amesema Manara.
“Ishu
ya kwamba tumemtoa nchi gani inakuwa siyo ‘story’ tena itakuwa
imeshapwaya hiyo. Watu wawe na subra Jumatatu siyo mbali”, ameongeza
Manara.
Juma
lililopita Manara alisema, wamepanga kumtangaza kocha mpya wiki hii
lakini Manara ametoa taarifa nyingine akisema kocha huyo atatambulishwa
wiki ijayo. Siku chache zilizopita, mwenyekiti wa usajili wa klabu hiyo
Zacharia Hans Poppe alisema, kocha waliyempata kurithi mikoba ya
Kopunovic ni raia wa Uingereza.