Mkuu
wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro
amelishtaki gazeti lililotangaza kuwa amefutwa kazi kwenye klabu hiyo
ambayo ndio mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu uliopita.
Muro amethibitisha kulipeleka mahakamani gazeti hilo na kudai fidia kutokan na upotoshaji huo uliofanyika dhidi yake.
“Ni
kweli msaidizi wangu Bw. Said Mbachiru alipeleka ‘demand’ kwenye gazeti
la Uhuru la kuwataka mambo matatu, jambo la kwanza ni wao kuandika
‘story’ kwa ukubwa uleule, ‘page’ ileile kukanusha kile walichokiandika.
Hoja nyingine ni kuwataka wao wanipe kiasi cha shilingi milioni 50 kama
usumbufu, halafu hoja ya tatu watoe ‘front page’ pamoja na maelezo
ambayo mimi nitayathibisha kuhusu walichokiandika wao, kwahiyo niseme
wazi tu kwenye hili hakuna kurudi nyuma”, amesema Muro.
“Hiyo
ni ‘demand’ ya kwanza kutoka kwa mwanasheria wangu, halafu wajiandae
kupata ‘demand’ nyingine ya pili kutoka kwa mwanasheria wa Yanga. Tangu
nimeingia Yanga sijawahi kupewa barua ya onyo, sijawahi kukaripiwa,
sijawahi kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu na maadili ya klabu na
hakuna kitu ambacho kimewahi kufanyika dhidi yangu kikionesha mimi
nimekuwa na utovu wa nidhamu”, alifafanua Muro.
“Nataka
kieleweke kitu kimoja, sisi ndani ya Yanga tunafanya kazi kama watu
wamoja, familia moja, lakini huenda ikawa watu ambao hawako ndani ya
uongozi wa Yanga wakawa wanakwazwa na kuumizwa na kauli zangu. Duniani
huwezi ukapendwa na watu wote na huwezi ukachukiwa na watu wote. Sasa
mimi nataka hao watu tukutane mahakamani, na nikwambie tu huyo mwandishi
aliyetoa hiyo habari atakwenda kusema mahakamani na kuthibisha mtu
aliyemwambia habari hizo, na hapo ndipo tutampata mchawi”, Muro
alilalama.
“Sikuzote
nimekuwa nikisema sikwenda Yanga kubembeleza ajira, katibu wetu siku
zote amekuwa imara akizungumza pasipo uoga, pasipo kificho, sisi
hatukwenda Yanga kuganga njaa na wale ambao walikuwa wapo Yanga kuganga
njaa safari yao imefika”, ameeleza.
“Unajua
kabla ya mtu kupewa uongozi inabidi kwanza apimwe akili, mimi
sikurupuki na kuzungumza vitu ambavyo vinatoka kichwani mwangu, watu
wanasema maneno ya Jerry makali lakini tunapokwenda kujenga mfumo huwezi
kujenga mfumo kwa kuchekea watu. Na wale wanaoona nakurupuka tu kusema
vitu ambavyo sijatumwa wakae wasubiri muda wangu wa uongozi uishe, na
ndio maana sisi kwetu Yanga kwanza mtu baadae”, alimaliza.
Awali
zilizagaa habari kuwa Jerry Muro ametimuliwa na uongoi wa klabu ya
Yanga na baadae taarifa hiyo ilionekana kwenye gazeti la Uhuru ikieleza
habari hiyo ya kutimuliwa kwa Muro kunako klabu ya Wanajangwani