Pamoja na kufanya jitihada za kumnasa
mshambuliaji Laudit Mavugo, Simba bado inadaiwa na Vital’O ya Burundi na
imekiri.
Vital’O inaidai Simba dola 5,000 (zaidi ya
Sh milioni 10) ikiwa ni sehemu ya fungu la usajili wa Amissi Tambwe.
Tayari Tambwe yuko Yanga baada ya Simba
kumtema, lakini bado hawajalipwa fedha hizo.
Taarifa za awali zilieleza kuwa deni hilo
limevuruga hata usajili wa Mavugo kwa Vital’O kutaka kulipwa kwanza fedha za
Tambwe.
Lakini uongozi wa Simba kupitia mjumbe wake
wa kamati ya utendaji, Collins Frisch ikatoa ufafanuzi kwamba la hasha.
“Hakika hilo deni lipo na tumelikubali hata
kama lilikuwa wakati wa uongozi uliopita, lakini Simba ndiyo hii,” alisema
Frisch.
“Lakini tumeelewana vizuri na Vital’O na tuko katika mchakato wa kulipa lakini hilo halijaingiliana na usajili wa Mavugo, si kweli.”