Mabingwa
wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga, Jumamosi ya wiki hii
wanashuka uwanja wa Taifa kuikabili SC Villa ya nchini Uganda kwenye
mchezo wa kirafiki wa kimataifa ikiwa ni mchezo wa hisani kwa ajili ya
kuchangia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
Katibu
mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, watautumia mchezo huo
kuwatambulisha wachezaji wao wapya watakao kipiga msimu ujao
“Mje
muwaone vijana wenu wapya ambao wameajiriwa Yanga na waliokuwepo
waliokuwa kwenye majukumu ya timu za taifa. Bahati nzuri ni kwamba,
Yanga yetu sisi kwa maana ya uongozi uliopo, ninyi wenyewe ni mashahidi
katika ardhi ya Tanzania sidhani kama kuna timu imekuja ikapata matokeo
mazuri zaidi ya Etoile du Sahel iliyopata ‘draw’ hapa, wengine wote
wamechezea visago tu”, ametamba Tiboroha.
“Mje
muangalie pia Jumamosi hiyo itakuwa nafikiri tunajaribu ku-copy na
ku-cut halafu tuna-pest mashindano ya kimataifa yaliyopita, tupo kwenye
maandalizi na niwahakikishie kwamba tupo ‘serious’ kwenye maandalizi
yetu, sasa ‘how serious’ tunajiandaa njooni muone Jumamosi kwa wingi
wenu bila kujali unatoka wapi”, amesema.
“Hii
ni ‘international game’ mje muangalie burudani, masuala ya ushabiki pia
muweke pembeni, mje muangalie game hii ni ya kijamii. Mkumbuke hata
ukiwa Simba, Coastal Union, Azam wala timu yoyote ya ‘premier’ ambayo ni
wapinzani wa Yanga. Hii sio ishu ya Yanga ni ishu ya jamii, kwahiyo
mnachotakiwa ni kuja kuangalia hiyo game lengo letu sisi ni kuhamasisha
uchangiaji wa hiki kituo Yanga hatuchukui hata shilingi kumi”,
maeongeza.
“Hamtokuja
kuiangalia Yanga ikicheza, mtakuja kusaidia jamii kwa kuwasaidia hawa
watoto wanaoshi kwenye mazingira magumu”, amesisitita..