Yanga
imekuwa timu iliyoanza mazoezi mapema ikilinganishwa na timu nyingine za Dar es
Salaam.
Kocha
Hans van der Pluijm amesema wataendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Karume,
Ilala.
"Ukianza
mapema, unakuwa na nafasi ya kuamua mambo mengi, ubadili nini au
uongeze kipi. Kuanza mapema pia kunasaidia wachezaji kuwa fiti zaidi,"
alisema.
Hata
hivyo Yanga imekuwa ikifanya mazoezi na baadhi tu ya wachezaji wake kwa kuwa
wengine wako katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, pia Rwanda.