MABINGWA wa Kandanda Tanzania bara, Young
Africans leo wanaendelea kujifua uwanja wa Karume, Dar es salaam ikiwa ni siku
ya tatu mfululizo tangu waanze maandalizi ya kujiwinda na ligi kuu msimu ujao,
kombe la Kagame na michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Yanga imekuwa timu iliyoanza mazoezi mapema ikilinganishwa na
timu nyingine za Dar es Salaam ambazo ni Simba na Azam fc.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm
amesema wataendelea kufanya mazoezi katika Uwanja wa Karume wakati huu
wanawasubiri wachezaji wote waliopo timu za taifa za nchi zao yaani Taanzania, Rwanda na
Burundi.
"Ukianza mapema, unakuwa na nafasi ya kuamua mambo mengi, ubadili nini au uongeze kipi. Kuanza mapema pia kunasaidia wachezaji kuwa fiti zaidi," amesema Pluijm.