Inapendeza zaidi! Ndilo neno pekee unaloweza kulitumia kuelezea hali ya kikosi cha Yanga kwa hivi sasa baada ya wachezaji wote kulipwa malimbikizo ya mishahara yao waliyokua wakiudai uongozi wa klabu hio na hivi sasa ni mwendo wa kanyaga twende.
Kikosi hicho kinaendelea na mazoezi yake jijini Dar es salaam ili kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaofuata mwishoni mwa juma hili dhidi ya Tanzania Prisons kutoka mkosani Mbeya mchezo utaochezwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Afisa Habari wa Klabu hio, Dismas Ten amesema kuwa kikosi hicho kipo katika hali nzuri hasa urejeo wa baadhi ya nyota wake waliokua majeruhi akiwemo Amissi Tambwe anaeendelea na mazoezi.
“Tunamshukuru Mungu, kikosi kipo katika hali nzuri, Tambwe amerejea kikosini, daktari amenithibitishia kuwa hali za wachezaji wengine wote ni nzuri, Prisons sio timu mbaya, ni timu nzuri hivyo tunajiandaa kukabiliana nayo,” alieleza Ten.
Yanga inaikaribisha Tanzania Prisons ikiwa na kumbukumbu murua ya ushindi mnono wa mabao 5-0 ilioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

AddThis

 
Top