Klabu ya Simba imetangaza kuwa mchezaji wao, Said Ndemla amepata nafasi ya kwenda nchini Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya AFC Eskilstuna.
Ndemla ambaye ni kiungo anayesifika kwa kupiga mashuti makali anatarajiwa kufanya majaribio hayo katika kipindi cha siku 14 na anatarajiwa kuondoka nchini Tanzania, kesho Jumanne.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wao Simba wanaamini Ndemla atafanikiwa katika majaribio hayo na kama ikiwa ni kinyume na hapo, atarejea nchini na kuendelea kuichezea Simba ambayo bado ipo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Manara amesema kitendo cha Ndemla kuruhusiwa kwenda kufanya majaribio katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden ni muendelezo wa Simba kuwapa nafasi wachezaji wao pindi wanapata fursa ya kucheza soka la kulipwa nje ya mipaka.

AddThis

 
Top