Timu ya Simba imesafiri kutoka Mbeya kwenda Katavi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao.
Simba ambayo jana iliifunga Mbeya City bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, itakuwa na maoumziko mafupi ya wiki moja kupisha mechi za kimataifa.
Kutokana na hali hiyo benchi la ufundi limelazimika kucheza mchezo wa kirafiki ili kuwaweka fiti wachezaji kabla ya mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons mnamo Novemba 18, mwaka huu. 
Mratibu wa Klabu ya Simba, Abbas Suleiman ameweka wazi kuwa wakiwa Katavi watacheza mchezo mmoja wa kirafiki utakaochezwa kesho kisha keshokutwa Jumatano watarejea Mbeya.
Wikiendi ijayo kutakuwa na michezo iliyopo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ambapo timu za taifa zitakuwa kazini.
Abbas ameongeza kuwa baada ya mchezo wa kirafiki watarejea Mbeya kuendelea na kambi ya maandalizi.

AddThis

 
Top