Mkufunzi wa waamuzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Leslie Liunda ambaye kitaaluma ni mwamuzi wa soka naye ameshindwa kusema moja kwa moja kama Kichuya alikuwa ameotea (offside) au hajaotea (onside) kabla ya kufunga.
“Kamera hazikuonesha vyema, offside inaamuliwa wakati mpira unapigwa si wakati wa kupokea mpira. Picha haioneshi vizuri wakati mpira unapigwa nafasi ya Kichuya ilikuwaje, hivyo tunapaswa kukubaliana na maamuzi ya mwamuzi msaidizi (assistant referee),” Leslie Liunda.
Ukiachana na mazingira ambayo Kichuya alifunga bao (yanatajwa kuwa tata) mjadala mwingine unaoendelea ni kuhusu mpira ulioguswa kwa mkono na Jonas Mkude akiwa kwenye eneo la penati, wapo wanaoamini kwamba mwamuzi alitakiwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penati kutokana na kitendo cha Mkude kuushika mpira lakini wapo wengine wanasema mpira ulifuata mkono.