Wakati Ligi Kuu ya Vodacom ikiwa imesimama kwa muda kupisha michezo ya kimataifa, kikosi cha Simba kilikuwa mjini Katavi kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na hilo likawezekana.
Ikiwa mjini hapo, Simba imecheza mchezo wa kirafiki dhdi ya Nyundo FC ya mjini Katavi ambapo kipute hicho kilipigwa kwenye Uwanja wa Azimio uliyopo Mpanda Mkoa wa Katavi, jana jioni na matokeo ni kuwa timu hizo hazikufungana.
Katika mchezo huo Simba iliwachezesha baadhi ya wachezaji ambao hawapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwenye michezo ya Ligi Kuu yha Vodacom huku Laudit Mavugo na James Kotei nao wakianza katika kikosi hicho.

AddThis

 
Top