Samatta aliumia goti Jumamosi iliyopita alipokuwa akiitumikia timu yake ya KRC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji ilipokuwa ikicheza dhidi ya Lokeren ambapo mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya 0-0.
Akizungumzia jeraha lake hilo, Samatta amesema baada ya kufanyiwa vipimo imegundulika mishipa midogo ya kwenye goti la kulia imechanika, hivyo atahitaji kufanyiwa upasuaji mdogo ili apone sawia.
Akifafanua zaidi, Samatta alisema: “Kuchanika kwa mishipa midogo ya goti, hivyo itachukua wiki sita au zaidi ili kupona, halafu kuna mshipa mwingine umepata tatizo, inatakiwa kufanyiwa upasuaji ndogo kuuweka katika hali nzuri ili isije kusumbua baadaye.” amesema.
Katika mchezo huo alioumia, Samatta alidumu uwanjani kwa dakika 40 kisha kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Nikolaos Karelis.
Kutokana na hali hiyo, Samatta ataukosa mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Benin, wikiendi hii inayokuja.