Ukurasa
wa mbele wa gazeti la The Sun leo umekuja na stori kwamba Manchester
United wanahitaji mshambuliaji wa maana ili kurudi kushindania ubingwa
msimu ujao.
Kwa mujibu wa The Currant Bun, "Manchester United wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic".
Mandzukic
ameibuka kuwa mchezaji anayewaniwa zaidi na Man United ili kutengeneza
muunganiko na Wayne Rooney msimu wa 2015/2016 chini ya kocha Louis van
Gaal.
United
wanalazimika kutafuta straika baada ya Radamel Falcao kurudi katika
timu yake ya Monaco, huku Van Gaal akiwa hana mpango wa muda mrefu na
Javier Hernandez na Robin van Persie.
Mario Mandzukic ni jibu kwa Van Gaal?
Mcroatia
huyo alianza kuonesha cheche akiwa Bayern Munich na msimu uliopita
alicheza vizuri akiwa na Atletico Madrid, lakini wachambuzi wengi wa
soka hawamuweki kwenye kundi la washambuliaji wa kiwango cha juu zaidi
duniani.
