Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameanza kukisuka kikosi chake kwa kuanza kuisuka kombinisheni mbili ya ushambuliaji katika kuhakikisha safu hiyo inakuwa tishio msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Maandalizi hayo yanawahusisha wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo ambao ni Deus Kaseke, Malimi Busungu na Benedicto Tinoco.
Kocha huyo alionekana akitengeneza kombinesheni hizo wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume juzi jijini Dar.
Kocha huyo alimuanzisha Busungu aliyecheza namba 10 na Mliberia, Kpah Sherman aliyecheza namba 9 ambao walionekana kucheza kwa kuelewana.
Kombinesheni hiyo, ilionekana kuelewana pale Busungu alipomtengenezea nafasi ya kufunga Sherman baada ya kugongeana ndani ya 18 kabla ya Mliberia huyo kufunga.
Kombinesheni ilionekana kunoga pale Busungu alipofunga bao la pili kwa kumchambua kipa akitumia krosi ya Sherman kabla ya kuzitingisha nyavu za Rangers.
Kipindi cha pili, kocha aliijaribu kombinesheni nyingine ya ushambuliaji kwa kumtoa Sherman na kuingia Mrundi, Amissi Tambwe aliyecheza pamoja na Busungu.
Washambuliaji hao, walionekana kuelewana kwa kutengenezeana nafasi za kufunga licha ya kushindwa kuzitumia vema nafasi hizo.
“Najaribu kombinesheni tofauti za wachezaji na pia nawapa mbinu huku nikiendelea kuwapa mazoezi ya nguvu na stamina,” alisema Pluijm mara baada ya mechi hiyo.

AddThis

 
Top