Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaendelea kujinoa
katika uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamika kama Haille Sellsie
uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu
fainali za mataifa ya Afrika 2017 utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.
Afisa.
Afisa habari wa Shirikisho la soka nchini TFF aliyeambatana
na timu hiyo huko Ethiopia, Baraka Kizuguto amesema kikosi cha Stars kinakwea
pipa kesho jioni kuwafuata Mafarao wa Misri.
“Timu inatarajia kuondoka kesho Ijumaa jioni
kuelekea Cairo, kwasasa bado timu inaendelea kufanya mazoezi hapa Addid Ababa
katika uwanja wa Taifa”. Amesema Kizuguto na kufafanua: “Leo jioni timu inafanya
mazoezi katika uwanja wa Taifa (Ethiopia) hali kadhalika kesho, lakini mara
baada ya mazoezi ya kesho kikosi kitasafiri kwenda Cairo, kikifika kitaunganisha
moja kwa moja kwenda Alexandria Jumamosi asubuhi kujiandaa na mechi itakayochezwa
jumapili”.