Baada ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuviagiza
vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara, kuhakikisha vinalipa kodi
kutokana na kuajiri makocha na wachezaji wanaocheza soka kutoka ndani na nje ya
Tanzania
Klabu ya Yanga kupitia kwa katibu wake mkuu Dkt. Jonas
Tiboroha wamesema suala hilo halina shida kwao kwasababu ni wajibu wa kila mtu
ambaye ameajiriwa Tanzania kulipa kodi, cha msingi ni kuangalia anapata kiasi
gani na anatakiwa kulipa kiasi gani ili isije kuwakatisha tamaa watu wanaofanya
kazi za mpira ikiwa ni wachezaji pamoja na makocha.
“Kwa ninachoelewa mimi, suala la kulipa kodi ni suala la
mchezaji binafsi au mtu binafsi alieajiriwa kwahiyo sioni kama ni tatizo kubwa
sana lakini ni suala la kukaa chini na kujipanga kuangalia nani anapata nini na
atoe nini”, amesema Tiboroha.
“Hilo suala nafikiri ni la kila mtu kama sijaelewa
vibaya, na inapofikia kwenye masuala ya kodi
inakuwa ni kitu cha lazima, kama ingekuwa ni haki basi ingekuwa ni haki
ya kila mtanzania kufanya hivyo na kila mtu anaeishi Tanzania akiwa anafanya
kazi. Cha msingi ni kuangalia kodi kiasi
gani inatakiwa ili isijekuwafanya vijana wakaona hakuna hata manufaa ya kucheza
mpira”, amsema.
Jana ilitoka taarifa kutoka kwa Kamshina wa TRA akiliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa katibu mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu nchini vinavyoajiri walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wahakikishe wanaweka kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia kuwaajiri