Muwania
nafasi ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais ambaye ni Naibu Waziri wa
Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba ameahidi kukuza mchezo wa soka
katika mkoa wa Tanga endapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano ili
kuleta heshima kwenye mkoa huo kama ilivyokuwa kwenye miaka ya 70.
Makamba
anataka kurejesha heshima ya mkoa wa Tanga kwenye soka ambayo
imetetereka kwa kipindi kirefu, ameongeza kuwa atahakikisha hamasa
inakuwepo kwa wale wote wanaopenda michezo na kusisitiza kuwa, timu
zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania kutoka mkoa huo inabidi zinyakue taji
la ligi hiyo.
“Tanga
ilikuwa inaheshimika, timu za hapa zilikuwa zinashinda zinashiriki ligi
kuu ya Tanzania na kuwa mabingwa, zinashiriki michezo ya Afrika. Tanga
tulikuwa tunaona timu kutoka nje, sasa tutarudidha hadhi na heshma ya
mkoa wa Tanga kwenye michezo”, amesema Makamba.
“Tumeanza
kwa kuzipandisha timu zetu mbili za Coastal Union na African Sports
lakini tuna timu ya tatu ya Mgambo tutahakikisha kwamba hamasa
inakuwepo”, amesisitiza.
Makamba
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bumbuli ametangaza nia ya kuwania
urais kupitia chama chake cha CCM na sasa yupo kwenye ziara akizunguka
mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kutafuta wadhamini.