Wanandinga Mohamed Hussein 'Tshabalala'  (Simba), Mrisho Ngassa (Yanga) na Simon Msuva (Yanga) wanachuana kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/20145 iliyoandaliwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
 
Kwa upande wa makocha, Goran Kopunovic (Simba), Hans vand der Pluijm (Yanga) na Mbwana Makata (Prisons) wanachuana kuwania tuzo ya kocha bora wa VPL.
 
Hafla ya utaoaji wa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League (VPL) msimu wa 2014/2015 inatarajia kufanyika leo katika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya,  jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.
 
Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 
Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :
 
1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
 Mohamed Hussein (Simba SC)
 Mrisho Ngasa (Young Africans)
 Saimon Msuva (Young Africans)
2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
 Shaban Hassan (Coastal union)
3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Goran Kopunovic (Simba SC)
 Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
 Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)
4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Israel Mjuni Nkongo
 Jonesia Rukyaa
 Samwel Mpenzu
5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mgambo JKT
 Mtibwa Sugar
 Simba SC

AddThis

 
Top